MAXI Nzengeli nyota wa Yanga mwenye spidi na uwezo wa kutoa pasi ndefu na fupi akiwa ndani ya uwanja ujanja wake wa kufunga mabao upo akiwa ndani ya 18.
Nyota huyo kacheza mechi tano za ligi akiyeyusha jumla ya dakika 309, katoa pasi moja ya bao na kujaza kimiani mabao matatu msimu wa 2023/24.
Kwenye upande wa kutoa pasi za mabao rekodi zinaonyesha kuwa ana zali akiwa nje ya 18 na ndani ya 18 kama ambavyo alifanya hivyo mchezo wa ligi dhidi ya KMC alipotoa pasi yake ya kwanza dakika ya 80 Agosti 23 akiwa nje ya 18.
Dhidi ya Geita Gold alifanya kazi yake aipendayo kutengeneza nafasi ya bao ilikuwa dakika ya 45 akiwa ndani ya 18 alitoa pasi yake ya pili.
Mabao yake yote matatu aliyofunga alikuwa ndani ya 18 alianza kwa kuwatungua JKT Tanzania mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Yanga wakakoma pointi tatu.
Ilikuwa dakika ya 78 alifungua akaunti ya mabao ndani ya ligi na dakika ya 86 aliongeza msumari wa pili kwenye mchezo mmoja huku kete yake ya tatu ikikutana na Geita Gold ilikuwa dakika ya 68.
Nzengeli kahusika kwenye jumla ya mabao matano ndani ya Yanga kati ya mabao 15 yaliyofungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.