SIMBA YAITISHA AL AHY

ZIKIWA zimesalia takribani siku nane kabla ya Simba hijacheza dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League, uongozi wa timu hiyo umesema watawaonesha wapinzani wao kwamba Simba ni timu ya aina gani.

Mhezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, kisha marudiano Oktoba 24, Misri.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, alisema wana malengo ya kuhakikisha wanakwenda kushindana na sio kushindwa, hivyo wana kila sababu ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ambao ni muhimu kwao kushinda.

“Tuna malengo makubwa ya kuhakikisha tunafanya vizuri katika mashindano haya mapya, hatuna malengo ya kwenda kushindwa wala kwenda kushiriki tu, bali kwenda kushindana haswa.

“Tunakwenda kushindana, tunataka kwenda kulionesha Bara la Afrika kuwa sisi ni timu kubwa ambayo ina malengo makubwa ya kutaka kufanya makubwa zaidi,” alisema kiongozi huyo.