NGOMA NYINGINE KWA MTIBWA SUGAR HII HAPA

KETE inayofuata kwa Mtibwa Sugar kwenye Ligi Kuu Bara ni dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine ikiwa ni mzunguko wa kwanza.

Ikumbukwe kwamba Mtibwa Sugar yenye Yassin Mustapha imetoka kupoteza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Singida Fountain Gate.

Tanzania Prisons nao wametoka kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba walipokuwa nyumbani.