Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch imeunganana na watoa huduma ulimwenguni kote kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja huku ikiahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi na zenye ubunifu kwa wateja wake ili kuongeza burudani pindi wanaposuka mikeka yao kwenye tovuti na App.
Akitoa salamu za heri kwa wateja na wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Parimatch Bwana Erick Gerald amesema kila tatizo ambalo linalokwamisha safari ya mteja ya ushindi wanalichukulia kwa uzito mkubwa kwasababu huyo ni mteja wao wa thamani.
“Kama mnavyojua sisi ndio kampuni ya kwanza ya michezo ya kubashiri yenye huduma kwa wateja wake saa 24 siku 7 za wiki, hii inaonyesha ni namna gani mteja wetu ni kipaumbele namba moja. Wateja wa Parimatch wanaweza kuendelea kuwasiliana na huduma kwa wateja saa 24 kila siku kupitia nambari
0800 787878 kwa msaada Zaidi”, amesema Erick.
Aidha, Mkurugenzi huyo aliwaomba watanzania kuendelea kuiunga mkono kampuni hiyo ambayo imedhamiria kuleta sura mpya kwenye sekta ya michezo nchini sambamba na kubadilisha maisha ya mtanzania mmoja mmoja kupitia programu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujishindia kitita cha Milion 100 kupitia
Parimatch Jackpot.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Huduma Kwa Wateja wa kampuni hiyo Bwana George Suya, amesema Parimatch inaendelea kujitolea kutoa kiwango cha huduma zenye ubora wa hali ya jii kwa wateja wake na wadau mbalimbali wa
kubeti bila ya kujali maeneo waliopo.
“Kama sehemu ya hatua za kurejesha fadhila na uaminifu wa wateja wetu, huwa tunafanya shughuli mbalimbali za kipekee na maalum kuwathamani wateja. Baadhi ya shughuli ni pamoja na kutoa zawadi katika kumbukizi zao za kuzaliwa, tiketi za kwenda kushuhudia michezo viwanjani bila ya kusahau bonasi kibao,” amesema George.
Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao!
Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya
Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.