MBABE WA KARIAKOO AMEFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

PRINCE Dube nyota wa Azam FC amefungua akaunti ya mabao dakika ya tano kwa kufunga bao dhidi ya Kitayosce.

Nyota huyo anayekipiga kwa matajiri wa Dar ni mbabe wa Simba kwa msimu wa 2022/23 kwa kuwatungua kwenye mechi za ligi zote mbili walipokutana.

Katika dakika 180 msimu wa 2022/23 Dube alikuwa akiwapa tabu Simba yenye maskani yake Kariakoo kwa kuwaokotesha mipira kwenye nyavu.

Licha ya kuwa ni mbabe kwa Simba alikwama kuitungua Yanga ya Nasreddine Nabi ambayo ilitwaa ubingwa.

Dube alipokutana na Yanga kwenye mechi za lifi mchezo wa mzunguko wa kwanza walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 na ule wa pili Azam ilipoteza mbele ya Yanga.

Ni Agosti 16 Dube alipachika bao hilo katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kwenye mchezo huo Feisal Salum aliyeibuka Azam FC akitokea Yanga alifungua akaunti pia ya mabao alitupia mabao matatu.