YANGA WAMEANZA KUIVUTIA KASI FAINALI

BAADA ya kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya fainali ya Ngao ya Jamii, kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi kuelekea fainali.

Dakika 90 Yanga ilikamilisha Agosti 9, 2023 kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ukisoma Yanga 2-0 Azam FC.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Clement Mzize dakika ya 88 na Aziz KI dakika ya 84.

Ikumbukwe kwamba nyota hao wote wa Yanga walitambulishwa mchezoni dakika ya 65 wakitokea benchi.

Ushindi wa penalti 4-2 waliopata Simba dhidi ya Singida Fountain Gate unawafanya wakutane na Yanga Agosti 13 kwenye mchezo wa fainali.