NI Kariakoo Dabi ndani ya Tanga inasubiriwa kwa shauku kutokana na kila mmoja kushinda kigingi cha kwanza cha nusu fainali.
Katika nusu fainali ya pili dakika 90 zilikuwa ni ngumu kwa nyota wote katika kucheka na nyavu kati ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate.
Ubao umesoma Simba 0-0 Singida Fountain Gate na kupeleka changamoto za penalti kuamua mshindi ambaye ni Simba.
Simba chini ya Roberto Oliveira ni penalti 4-2 Singida Fountain Gate huku ile penalti ya kwanza ikiokolewa na Ally Salim mpigaji akiwa ni Aziz Andambwile.
Mpigaji wa penalti ya Simba alikuwa ni Luis Miquissone alieytokea benchi na kupachika bao kwenye mkwaju wa penalti uliomshinda Beno Kakolanya.
Agosti 13, Uwanja wa Mkwakwani ni Yanga v Simba fainali ya Ngao ya Jamii.