AZIZ KI MTAALAMU KAMILI GADO KWA FAINALI

AZIZ KI mtaalamu wa mapigo huru ndani ya kikosi cha Yanga Agosti 9 akitokea benchi alitupia bao moja dhidi ya Azam FC dakika ya 84.

Yanga imeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya fainali katika Ngao ya Jamii, Tanga.

Huo ulikuwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali alipomtungua kipa namba tatu wa Azam FC, Zuber Foba.

Foba hakuwa na bahati dakika ya 88 alitunguliwa bao la pili na Clement Mzize akiwa nje ya 18 nyota huyo wa Yanga.

Mabao hayo mawili yanaipeleka Yanga fainali ya Ngao ya Jamii inayotarajiwa kuchezwa Agosti 13 Uwanja wa Mkwawani, Tanga.

Ushindi wa Simba leo kwa penalti 4-2 dhidi Singida Fountain Gate umewapa tiketi ya kutinga fainali.

Sasa ni Kariakoo Dabi ndani ya Mkwakwani, Tanga.