AZAM FC NI MASHUHUDA WA FAINALI TANGA

AZAM FC watakuwa mashuhuda wa fainali Agosti 13 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kugotea hatua ya nusu fainali ya kwanza kwa kupoteza mbele ya Yanga.

Licha ya kuanza kwa kasi Agosti 9 dhidi ya Yanga waliambulia maumivu kwa kupoteza mazima mchezo huo dhidi ya Yanga.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilitwaa taji ya Ngao ya Jamii 2022 kwa ushindi wa mabao 2-1 Simba mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwa kufungashiwa virago hatua ya nusu fainali ya kwanza sasa watasubiri mwingine atakayefungashiwa virago kwenye nusu fainali ya pili.

Ni Simba v Singida Big Stars hawa wataamua nani atacheza fainali na nani atacheza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.

Agosti 13 2023 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ambapo mabao ya Yanga yalifungwa na Aziz KI dakika ya 84 na Clement Mzize dakika ya 88.