NDONDO CUP KUNA SHIDA

UONGOZI wa Chama cha Soka Ubungo (UFA) umeweka wazi kuwa kumekuwa na changamoto ya viwanja katika uendeshaji wa mashindano ya Ndondo Cup ambayo yanaendelea jijini Dar.

Shida hiyo ya viwanja inawafanya wachezaji kukwama kutoa ile burudani kwa mashabiki kwa kiwango cha juu kutokana na kuhofia kupata maumivu.

Ikiwa ni muendelezo wa 32 Bora ambapo timu 32 za Ndondo zinajinoa vilivyo na mashindano mazima yakisimamiwa na Chama Cha Soka Dar (DRFA).

Ndondo Cup imekuwa ikifuatiliwa na wengi kutokana na uwekezaji wake na namna ambavyo vijana wanaupiga mwingi wakiwa uwanjani.

Katibu Mkuu wa UFA, Frank Mathew amesema licha ya kuwa mashindano haya yanawadhamini lakini bado kuna changamoto mbalimbali hususan kukosa walimu wenye ujuzi.

“Mbali na hilo changamoto kubwa ni uhaba wa viwanja na vilivyopo havina ubora wa kutosha hivyo huhatarisha afya za wachezaji.”