KUELEKA kwenye Simba Day Agosti 6 2023 Dr Shabiki wa Simba amebainisha kuwa Yanga wana mpango wa kuvuruga tamasha hilo.
Yanga imekamilisha jambo lao kwa kuwatambulisha wachezaji wapya kwa ajili ya kuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24. Yanga imewatambulisha Max Zengeli, Skudu ambao wanaingia kwenye kikosi cha Yanga inayonolewa na Miguel Gamondi.
Yanga wana mpango kazi wao wa kuzindua documentary inayotarajiwa kuzinduliwa Jumatatu.
Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe ameweka wazi kuwa ni historia inakwenda kukamilika kutokana na jambo hilo.