UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa kazi kubwa watafanya kwa msimu mpya wa 2023/24 wana imani na wachezaji wao wapya pamoja na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2022/23.
Leo Agosti 3 mastaa wa Simba wanatarajiwa kuanza maandalizi kwa ajili ya Simba Day inayotarajiwa kuwa Agosti 6.
Mastaa wapya ndani ya kikosi cha Simba ni pamoja Fabrice Ngoma, Luis Miquissone, Idd Chilunda na kipa mpya Jefferson ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi baada ya kuumia.
Singida Fountain Gate Agosti 2 walikamilisha jambo lao kwa kuwatambulisha nyota wapya na wale ambao walikuwa katika kikosi hicho kwa msimu wa 2022/23.
Yanga jambo lao tayari limeshakamilika ilikuwa ni Wiki ya Mwananchi na walicheza na Kaizer Chiefs.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kila kitu kipo kwenye mpangilio mzuri watapambana kupata matokeo chanya.
“Ni bandika bandua kwenye mashindano ambayo tunashiriki kitaifa na kimataifa malengo yetu ni kuona kwamba tunafanya vizuri na kuwapa burudani mashabiki wetu wa Simba ulimwenguni kote.
“Kikubwa ambacho tunakifanya ni kuwa na maandalizi mazuri kwenye kila sekta tupo tayari na kazi itaanzia kwenye Ngao ya Jamii hakika tabasamu litazidi kwenye mechi zetu ambazo tutacheza,” amesema.
Simba iliweka kambi Uturuki ambapo huko ilicheza mechi za kirafiki za kimataifa.