YANGA KAZI INAENDELEA, KETE YAO YA KWANZA HII HAPA

MCHEZO wa kwanza wa Yanga kwenye ushindani ndani ya msimu wa 2023/24 ni dhidi ya Azam FC.

Huu utakuwa mchezo wa ufunguzi katika hatua ya Ngao ya Jamii ikiwa ni mfumo mpya utatumika.

Ni mwendo kama wa ligi na timu nne zitashiriki zile zilizogotea nafasi nne za juu ikiwa ni Yanga ambao ni namba moja, Simba namba mbili.

Azam FC namba tatu huku Singida Big Stars kwa sasa ni Singida Fountain Gate iligotea nafasi ya nne.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Azam FC, Uwanja wa Mkwakwani Tanga Agosti 9 2023 na ikumbukwe kwamba ni wao walitwaa Ngao ya Jamii msimu wa 2022/23 kwa kuwatungua Simba mabao 2-1.

Miongoni mwa nyota ambao wameanza mazoezi na Yanga iliyoweka kambini Avic Town Kigamboni kwa Yanga ni Mudhathir Yahya, Khalid Aucho, Jonas Mkude.

Yanga ipo chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi ambaye amerithi mikoba ya Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.