NIDHAMU MSINGI WA MAFANIKIO KWA WACHEZAJI

USHIRIKIANO kwenye kazi ambazo zinafanywa kwa sasa ni muhimu kwenye kila jambo na hii inaongeza nguvu kwenye kupata matokeo chanya.

Mabingwa msimu wa 2022/23 Yanga wana kazi kubwa kufikia malengo yao kwa msimu mpya.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilipata mafanikio kwa kutwaa mataji mengine ikiwa ni Kombe la Azam Sports Federation na Ngao ya Jamii.

Pia Yanga inakwenda kushiriki Ligi ya mabingwa huku Singida Fountain Gate na Azam FC hawa watakuwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Kila mmoja anahitaji kupata ushindi na hii inaleta picha nzuri kwa ajili ya mechi zote ambazo zinatarajiwa kuchezwa kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wale ambao wameweka kando malengo ya msimu uliopita kwa kushindwa kuyafikia ni muda wa kutazama upya mipango iliyopita na kuanza kusonga mbele.

Kikubwa ni kuangalia namna ambayo malengo yaliyopo na yale yanayofuata yatakavyopewa kipaumbele hilo ni jambo la msingi kwenye kila idara kuanzia Championship, Ligi ya Wanawake na ligi ya mikoa.

Siku zinapita kwa kasi kuelekea pale ambapo ligi inakwenda kuanza hivyo ni muda wa kukamilisha mipango yote kwa sasa na hii ni muhimu.

Kuanzia kwenye usajili kwa wakati huu ni muhimu kukamilisha taratibu zote ili kuanza maandalizi kwenye kila idara kuwa tayari msimu utakapoanza.

Zile ambazo hazijakamilisha usajili muda uliopo ni sasa kabla ya dirisha la usajili kufungwa wakiwa wamebaki na wachezaji wao waliokuwa nao msimu uliopita kwa upande wa anga la kimataifa.

Kusubiri mpaka dirisha dogo ili kuongeza nguvu hapo kutakuwa na shida kwani muda bado upo ikiwa kuna mambo hayajakamilishwa ni sasa.

Maandalizi yakianza mapema yanatoa picha kwa wakati ujao namna itakavyokuwa kwenye timu zote ambazo zinashiriki mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Wale wenye nafasi ya kushiriki kimataifa wameshaanza kupata picha ya namna washindani wao watakavyokuwa kwenye mechi zote hilo ni jambo la msingi.

Iwe wanaanzia nyumbani ama ugenini kitu cha msingi ni kupambana kwa umakini na kupata matokeo mazuri hilo litaongeza nguvu ya kujiamini na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Mbinu za ushindi zitawapa nguvu ya kusonga mbele hivyo kila mchezo una umuhimu iwe ni nyumbani ama ugenini.

Kila kitu ili kiwe bora na chenye kuvutia kwenye maisha ya soka kinahitaji maandalizi mazuri hivyo tu basi.

Muhimu kila mmoja kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa umakini na muda uliopo ni sasa hakuna ambaye anapenda kupata matokeo mabaya.

Pia ni muhimu wachezaji kuongeza nidhamu wawapo eneo la mafunzo na wakiwa nje ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza viwango vyao.

Nidhamu ni kitu cha muhimu katika kutimiza majukumu yote na inaongeza uelewa hata pale ambapo mchezaji anakuwa hajaelewa inakuwa rahisi kwa benchi la ufundi kumpa mbinu nyingine zaidi.

Kuanzia kwa wachezaji ni muhimu kuwa tayari kwenye muda wa maandalizi hiyo itawaongezea hali ya kujiamini na nguvu ya kupambana kwenye kutafuta matokeo.

Furaha ya mashabiki ipo kwenye matokeo mazuri ambayo yanapatikana uwanjani hivyo kwa kutimiza majukumu kwa umakini kunaongeza nguvu ya mashabiki kuzidi kujitokeza uwanjani.

Hamasa kubwa ambayo inafanyika kwa mashabiki itakuwa endelevu ikiwa matokeo yatakuwa yanapatikana uwanjani kutoka kwa wachezaji.

Mchezo wa makosa unahitaji umakini kwenye kutendea kazi katika kila hatua ambayo inakuwa inafanyika kwenye uwanja wa mazoezi.

Sio Ihefu pekee bali hata Namungo, Kagera Sugar nao ni muhimu kufanya maandalizi mazuri.

Ushindani ni muhimu kwa kuwa unafanya ligi iwe inavutia na kila timu kuhitaji kuonyesha kileilichonacho kwa mashabiki na ulimwengu wa mpira.

Wachezaji ni muda wa kuonyesha uwezo wenu wakati huu wa maandalizi itaongeza nafasi ya kujiamini hata kabla ya ligi kuanza.

Muhimu kuongeza ushirikiano kwa benchi la ufundi na wachezaji wengine ndani ya timu hii ni muhimu pia kila wakati.