KUELEKEA Singida Big Day inayotarajiwa kufanyika Agosti 2, Uwanja wa Liti uongozi wa Singida Fountain Gate umetambia jambo lao kuwa litakuwa na upekee kwenye kila hatua.
Ni burudani kwa mashabiki wa Singida Fountain Gate ambapo wanakwenda kutambulisha kikosi rasmi kwa msimu wa 2023/24 na benchi jipya la ufundi.
Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa huku wachezaji wakiwa tayari kuonyesha uwezo wao.
“Jambo letu linakwenda sawa na kila kitu kipo kwenye mpangilio ikumbukwe kwamba kutakuwa na burudani za kutosha pamoja na sapraizi nyingi.
“Kuna wachezaji watakwenda kutambulishwa ambao watakuwa katika kikosi kwa msimu mpya hili ni kubwa na muhimu kwa mashabiki kujitokea uwanjani kushuhudia haya yote kwa ajili yao na kiingilio kwa mzunguko ni 3,000 huku VIP ikiwa ni 5,000,” amesema Massanza.