WAKATI tetesi zikieleza kuwa kiungo mkabaji ingizo jipya ndani ya YangaJonas Mkude amesepa kambini AVIC habari za kuamini zimebainisha kuwa nyota huyo yupo kambini.
Ikumbukwe kwamba Mkude ni ingizo jipya ndani ya Yanga aliibuka hapo akiwa mchezaji huru baada ya kukutana na Thank You kutoka kwa mabosi wake wa zamani Simba.
Aliibuka hapo akiwa mchezaji huru na alikuwa miongoni mwa kikosi cha Yanga kilichocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs akikomba dakika 45.
Taarifa kutoka chanzo cha kuamini ndani ya Yanga zimeeleza kuwa Mkude yupo kambini akiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.
“Hizo taarifa kuhusu Jonas Mkude kutokuwepo kambini hazina ukweli wowote hayo ni maneno labda wale ambao wanasema hivyo walimuona siku moja akiwa hayupo kasha wakafikiri ni siku zote hayupo.
“Kweli Mkude alikosekana siku moja lakini aliomba ruhusa kisha akarudi kwa ajili ya kuendelea na program nyingine hivyo tu basi,” ilieleza taarifa hiyo.
Championi Jumamosi lilipomtafuta Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema;”Mimi siwezi kutoa taarifa kwa sasa labda ikitokea imetakiwa iwe hivyo idara ya habari inashughulikia masuala yote ya kutoa taarifa,”.