BANGALA AKUTANA NA THANK YOU YANGA

YANICK Bangala beki aliyekuwa ndani ya Yanga msimu wa 2022/23 amekutana na Thank You.

Ni Julai 29 taarifa rasmi kutoka Yanga imeeleza kuwa nyota huyo hatakuwa kwenye kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24.

Taarifa hiyo imeeleza namna hii: “Uongozi wa Young Africans SC unapenda kuutarifu umma kuwa tumefikia makubaliano na Klabu ya Azam FC ya kumnunua mchezaji wetu Yannick Bangala,”.

Bangala hakuwa sehemu ya wachezaji waliotambulishwa ndani ya Yanga kwenye Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Mkapa.

Hivyo kwa taarifa hiyo Bangala ambaye ni kiraka atakuwa ni nyota mpya ndani ya Azam FC ambayo imeweka kambi Tunisia.

Ni mkataba wa mwaka mmoja alikuwa amebakiza ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Migueli Gamondi.

Anaungana na Feisal Salum ambaye naye alikuwa Yanga msimu wa 2022/23 wa sasa yupo ndani ya Azam FC naye pia Yanga walifanya mazungumzo na Azam FC kuhusu kumpata Feisal.