HABIB Kondo ni kocha mpya ndani ya Mtibwa Sugar kwa msimu wa 2023/24 tayari ameanza kazi rasmi.
Kocha huyo ana uzoefu na soka la Bongo aliwahi kuifundisha KMC yenye maskani yake Kinondoni.
Timu hiyo kambi yake ipo kwenye mashamba ya milima ya miwa pale Morogoro, Manungu.
Mtibwa Sugar inatumia Uwanja wa Manungu kwa mechi zake za nyumbani.