YANGA KAMILI GADO KAZIKAZI

CHINI ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Yanga inaendelea na mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.

Ni AVIC Kigamboni Yanga imeweka kambi ikiwa na maingizo ya wachezaji wapya pamoja na wale waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2022/23.

Tayari Yanga imeshafanya utambulisho wa wachezaji wao ikiwa ni pamoja na Nickson Kibabage ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Singida Fountain Gate.

Kwa wazawa wapo Dickson Job beki wa mpira mwenye tuzo ya beki bora ndani ya ligi msimu wa 2022/23.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Asas FC ambapo itaanzia ugenini na itamalizia nyumbani.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Agosti 18 2023.