JULAI 25 droo ya CAF kwa timu ambazo zinazoshiriki mashindano kimataifa imechezwa leo ambapo wawakilishi wa Tanzania bara na visiwani wamewatambua wapinzani wao.
Ni Yanga washindi wa pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022/23 wao wataanza katika raundi ya kwanza.
Klabu ya Yanga chini ya Miguel Gamondi mrithi wa mikoba ya Nasreddine Nabi ataongoza kikosi hicho kusaka ushindi dhidi ya ASAS FC ya nchini Djibouti kwenye Raundi ya ya Kwanza ya Mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
Timu ya Yanga tayari imeshatambulisha wachezaji wake wapya na wale iliokuwa nao kwa msimu wa 2022/23.
Miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa na kazi kwenye anga la kimataifa ni makipa Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja, Metacha Mnata kipa namba mbili na Aboitwalib Mshery.