VIINGILIO VYA SIMBA DAY HIVI HAPA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa siku ya Simba Day ni sikukuu hivyo hawapangi viingilio vikubwa kuwakomoa mashabiki wao.

Agosti 6 ni Simba Day ikiwa ni siku ya utambulisho kwa wachezaji pamoja na benchi jipya la ufundi pamoja na lile lililokuwa na timu msimu wa 2022/23.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema lengo kubwa ni kila mmoja kupata burudani na kuwaona wachezaji wakiwa uwanjani.

“Kwa upande wa viingilio, sisi kama klabu tunahitaji fedha lakini kwenye tamasha tunahitaji zaidi mashabiki, Wanasimba waje zaidi ndio maana tunawatafuta wadhamini wa kusaidia gharama. Tunajali zaidi maslahi ya Wanasimba.

“Viingilio vya Simba Day ni Platinum – Tsh. 200,000, VIP A – Tsh. 40,000, VIP B – Tsh. 30,000, VIP C – Tsh. 20,000, Machungwa – Tsh. 10,000 na Mzunguko – Tsh. 5,000.

“Kispika kinarudi mtaani kuwaita Wanasimba kwenye Simba Day. Tunaenda kuwaonyesha kwamba Uwanja wa Mkapa ni mdogo sana kwa Simba kuujaza,” amesema.