WENGINE KUUZWA SIMBA BAADA YA SAKHO

BAADA ya kumuuza Pape Sakho Simba wamesema kuwa mchezaji yoyote yule watamuuza ikiwa watapata ofa nzuri.

Julai 24 timu hiyo ambayo imeweka kambi Uturuki ilicheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Zira.

Katika mchezo huo walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Miongoni mwa wachezaji waliopo Uturuki ni pamoja na Clatous Chama,Fabrice Ngoma, Kibu Dennis ambaye alifunga bao kwenye mchezo huo.

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema kuwa wachezaji wake wanazidi kuimarika taratibu.

Chama ameibuka Uturuki baada ya kuwa kwenye mvutano na uongozi wa Simba kuhusu mkataba wake ambapo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga.

Mwisho Chama alifikia makubaliano na Simba kuendelea kubaki hapo na kukwama kwa dili lake la kueleka Yanga.

Wakati Chama akibaki Simba kiungo Jonas Mkude Legend ndani ya soka anaibukia Yanga akitokea Simba.

Mkude mkataba wake uligota mwisho hivyo anaibuka ndani ya Yanga akiwa ni kiungo huru.

Sakho raia wa Senegal ameuzwa kwenda Quevilly Metropole FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Ufaransa.