PAPE SAKHO HUYO ULAYA

RASMI Simba SC imefikia makubaliano na Klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa kumuuza mchezaji Pape Sakho.

Kiungo huyo ni miongoni mwa viungo bora wenye mambo mengi ndani ya uwanja akiwa na mtindo wa ushangiliaji wa kunyunyiza.

Moja ya mabao aliyofunga ndani ya Simba ilikuwa dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Simba.

Mabao kwa Yanga yalifungwa na mshambuliaji Fiston Mayele raia wa DR Congo.