HAYA HAPA KUTEKA SHOW SIKU YA SINGIDA FOUNTAIN GATE DAY

MIPANGO mikubwa ndani ya Singida Fountain Gate inayoshiriki Ligi Kuu Bara inaendelea ikiwa ni pamoja na siku maalumu ya utambulisho wa wachezaji wao pamoja na benchi la ufundi.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 ilikuwa inaitwa Singida Big Stars na ilikuwa inatumia Uwanja wa Liti kwa mechi za nyumbani.

Msimu wa 2023/24 itakuwa ni Singida Fountain Gate baada ya kufanyiwa mabadiliko kwa kuuza hisa kwa mmiliki mwingine ila ngome ipo palepale Singida.

Kuelekea kwenye tamasha hilo la Singida Fountain Gate ambalo linatarajiwa kuwa ni Agosti 2 2023 kuna mambo matano makubwa ambayo yatafanywa katika siku ya tukio.

Haya hapa yatakayofanywa siku ya Singida Fountain Gate:-

1. Utambulisho wa kikosi kilichoboreshwa
2. Utambulisho wa Benchi la Ufundi
3. Mechi za utangulizi ikiwemo za wanawake.
4. Burudani kutoka kwa msanii mkubwa wa Bongo Fleva
5. Mechi kali ya kimataifa (International Friendly Match)

Ikumbukwe kwamba tayari Singida Fountain Gate imetambulisha uzi mpya kwa ajili ya msimu wa 2023/24.