KIPA MPYA SIMBA HUYU HAPA

RASMI Klabu ya Simba imetangaza nyota Jefferson Luis raia wa Brazil kuwa kipa mpya ndani ya timu hiyo.

Kipa huyo ni nyota wa 10 kusajiliwa ndani ya Simba ambayo imeweka kambi Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Alikuwa anacheza Klabu ya Resende FC ya Serie D ya Brazil na msimu uliopita alicheza kwa Mkopo katika Club ya Itabirito FC-MG.

Anaungana na Ally Salim ambaye ni kipa namba tatu pamoja na Aishi Manula huyu ni kipa namba moja wa Simba.