MCHEZO wa kimataifa wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Kaizer Chiefs umekuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kuonyesha ushindani.
Dakika 45 zile za mwanzo ubao wa Uwanja wa Mkapa Yanga 1-0 Kaizer Chiefs.
Bao la uongozi limepachikwa na mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda dakika ya 45.
Musonda amepachika bao hilo akitumia pasi ya Maxi Nzengeli ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga.
Ukuta wa Yanga chini ya nahodha Bakari Mwanyeto umekamilisha dakika 45 ukiwa haujaokota bao kwenye nyavu zao.
Yanga na Kaizer Chiefs wamekiwasha ukiwa ni mchezo wa maandalizi kwa msimu wa 2023/24.
Kipindi cha pili wachezaji wote wa Yanga wa ndani walibadilishwa na nyota wapya ikiwa ni Gift Fred, Yao walianza huku kipa pekee Metacha Mnata akiendelea katika dakika za 45 kipindi cha pili.