KOCHA Mkuu Youssouph Dabo wa Azam FC amesema kuwa anawapa mbinu mpya wachezaji wake zitakazowafanya wawe wakomavu wa fikira.
Timu hiyo ipo kambini nchini Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.
Ipo wazi kwamba Azam FC ni mashuhuda wa taji la ubigwa wa ligi msimu wa 2022/23 likiwa ni mali ya Yanga.
Katika Ngao ya Jamii walifika fainali na kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ukisoma Azam FC 0-1 Yanga.
Dabo ambaye ni raia wa Senegel amesema ameona sehemu ambayo wachezaji wake bado hawajawa imara sana ni eneo hilo jambo ambalo wanalifanyia kazi.
“Wachezaji wanajituma na ninafurahi wanafuata maelekezo ambacho kipo kwa sasa ni kwenye kuwaongezea mazoezi ya ukomavu wa fikra jambo ambalo kwao lilikuwa chini sana kwenye eneo hilo.
“Ambacho kinafanyika kwa sasa ni kuendelea kuangalia maeneo mengine zaidi ikiwa ni pamoja na kuwapa mazoezi magumu ili wazidi kuwa imara,” amesema.