RASMI Luis Miquissone ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba ambacho kimeweka kambi Uturuki kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.
Nyota huyo ni chaguo la mashabiki ambao walipewa chaguo la kumtaja nani ambaye atarejea kwa kuwa alibaki mmoja kati ya wawili ambao Simba ilipanga kuwarejesha.
David Kameta ambaye ni beki huyu alianza kisha swali likabaki ni nani atakuwa wa pili ndani ya Simba.
Hatimae leo Julai 22 ametambulishwa Luis aliyekuwa ndani ya Al Ahly ambapo huko alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mabosi wake hao.