MTU TATU NDANI YA SIMBA, KULA CHUMA

MTU tatu kwa mpigo zimetambulishwa ndani ya Simba rasmi baada ya kusaini dili jipya kuwa kwenye familia ya Msimbazi.

Ni leo Julai 20 watatu wametangazwa kwa ajili ya kuwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Roberto Oliveira.

Ni kiungo Idd Chilunda ambaye alikuwa ndani ya Azam FC lakini hakuongezewa mkataba wake kwa sasa atakuwa ndani ya Simba.

Miongoni mwa wazawa wenye uwezo wa kutumia mguu wa kulia kwa umakini kwenye kutengeneza nafasi na kufunga akiwa uwanjani.

Mbali na huyo pia Hussein Abeid huyu ni beki ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Geita Gold pia amewahi kucheza Polisi Tanzania.

Mwingine ni kiungo mshambuliaji Abdalah Hamisi wote hawa ni nyota wapya ndani ya kikosi cha Simba.