YANGA HAWANA JAMBO DOGO BALAA LAO LINAENDELEA

NYOTA kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Pacome Zouzoua ni mali ya Yanga.

Nyota huyo ametambulishwa kuwa ni njano na kijani Julai 19,2023.

NI miongoni mwa nyota wa Yanga wanaotarajiwa kuonyesha makeke kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kaizer Chiefs.

Itakuwa Wiki ya Mwananchi Julai 22 2023 Uwanja wa Mkapa ikiwa ni siku ya utambulisho wa wachezaji wapya na wale ambao walikuwa kwenye kikosi hicho cha Yanga.

Miongoni mwa nyota ambao wametambulishwa na Yanga ni pamoja na Jonas Mkude, Nickson Kibabage, Skudu.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani utakuwa mkubwa msimu ujao jambo linalowafanya wazidi kuboresha timu hiyo.

“Tupo tayari kwa ushindani wa msimu mpya na tunafanya maandalizi ili tuendelee pale ambapo tuliishia, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.