NI Mahlatse Manoka Makudubela ni nyota mwenye uwezo mkubwa akiwa ndani ya uwanja kutokana na kumiliki, kutoa pasi na chenga za kukera atakuwa Jangwani.
Huyu ndiye atakayepewa namba sita ndani ya kikosi cha Yanga.
Ikumbukwe kwamba jezi hiyo ilikuwa mikononi mwa Feisal Salum ambaye yeye msimu ujao hatakuwa ndani ya Yanga bali Azam FC.
Nyota huyo maarufu kwa jina la Skudu ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Miguel Gamondi ambaye ni kocha mkuu.
Rasmi ametambulishwa Yanga Julai 19 saa sita usiku akiwa ni mchezaji aliyesubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa Yanga.
Wengine ambao wameshatambulisbwa ni Jonas Mkude, Nickson Kibabage na Gift Fred.
Timu hiyo inafanya maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2023/24 huku wakiwa na kazi ya kutetea taji la ligi ambalo Yanga walitwaa msimu wa 2022/23.
Julai 22 Yanga ina mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Wiki ya Mwananchi.