HUYU HAPA KOCHA MPYA YANGA

Taibi Lagrouni ametambulishwa kuwa kocha wa mazoezi ya viungo ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kimeanza maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2023/24.

Ni AVIC Kigamboni illipo kambi ya timu hiyo ya Yanga inayonolewa na Miguel Gamondi mrithi wa mikoba ya Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.

Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara baada ya kuongoza ligi msimu wa 2022/23 hivyo wana kazi ya kuendelea pale ambapo wameishia.

Julai 17 kocha huyo ametambulishwa ndani ya Yanga kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya timu hiyo kwa msimu mpya.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya Wiki ya Mwananchi inayotarajiwa kufanyika Julai 22, Uwanja wa Mkapa na itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.