Skip to content
MTAALAMU wa mapigo huru ndani ya kikosi cha Ihefu FC Nivere Tigere bado yupo ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2022/23.
Ihefu ni timu ya kwanza kuifunga Yanga msimu wa 2022/23 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Hiyo iliandikwa rekodi baada ya Yanga kucheza mechi 49 mfululizo bila kufungwa.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Highland Estate bao la Yanga lilifungwa na Yannick Bangala.
Kwa Ihefu ni Tigere alipachika bao la kwanza kwa pigo huru kisha akatoa pasi ya bao kwa Lenny Kissu aliyepachika bao la ushindi.
Bado yupo ndani ya Ihefu FC baada ya kutagazwa kuwa ameongeza mkataba na mabosi hao wa Mbeya.
Ikumbukwe kwamba ubingwa wa 2022/23 upo mikononi mwa Yanga huku Simba wakigotea nafasi ya pili.