RASMI Fabrice Ngoma ambaye ni kiungo ametambulishwa kuwa mali ya Simba.
Nyota huyo anakuja kuungana na wachezaji wengine kwa ajili ya kupambania malengo ya msimu wa 2023/24 na timu imeweka kambi Uturuki akijua kuwa ubingwa msimu wa 2022/23 upo kwa Yanga.
Alikuwa anatajwa kuwa kweye rada za Yanga pamoja na Azam FC ila Simba wanatajwa kufanikisha mpango wao wa kuinasa saini yake.
Ni amenunuliwa kutoka kutoka Al-Hilal ya Sudan hivyo anakuja kuanza changamoto mpya ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo wanatarajia kuanza na Singida Fountain Gate kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Tanga.