ABDI Hamid Moallin ni kocha mpya ndani ya kikosi cha KMC chenye ngome yake pale Kinondoni.
Kocha huyo ambaye amewahi kuifundisha Azam FC amerejea kwa mara nyingine kwenye ardhi ya Bongo.
Safari hii atakuwa na KMC kuipambania ndani ya Ligi Kuu Bara msimu mpya ujao.
KMC haikuwa na mwendo mzuri ndani ya msimu wa 2022/23 ilipata nafasi ya kubaki ndani ya ligi kwa mchezo wa mtoano.
Kocha huyo amesema kuwa hiyo kwake ni fursa anaamini atafanya kazi kwa ushirikiano ili kupata matokeo chanya.
“Tunaamini kuwa utakuwa ni msimu mzuri na ligi ina ushindani mkubwa hivyo tutapambana na kufanya kazi kwa ushirikiano hii kwangu ni fursa nzuri,”.