AZAM MATIZI KAMA YOTE TUNISIA

KIKOSI cha Azam FC kinaendelea na mazoezi Tunisia ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.

Timu hiyo ipo na wachezaji wake wapya ikiwa ni pamoja na Feisal Salum ambaye alikuwa ndani ya Yanga, Gubril Sillah ambaye ni kiungo.

Sillah amesema kuwa ni furaha kuwa na timu hiyo na anaamini watafanya kazi kubwa msimu ujao.

‘Nina furaha kuwa na wachezaji wenzangu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya nina amini kwa ushirikiano tutafanya kazi kubwa na nzuri  na ninaona ni wachezaji wazuri.

“Ninaona wachezaji wanapenda kujifunza kwa namna ambavyo tunafanya hakika tutakuwa na timu bora,”

Mchezo wao watakaporejea Bongo ni dhidi ya Yanga ambao ni hatua ya nusu fainali Ngao ya Jamii na fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 13, Tanga Uwanja wa Mkwakwani.