SIMBA HAO NDANI YA UTURUKI

MSAFARA wa Simba unaonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira leo Julai 11 umeanza safari kueleka Uturuki.

Ni maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24 unaotarajiwa kuanza Agosti ambapo kwa msimu wa 2022/23 walipishana na ubingwa uliokwenda Yanga.

Simba ina kazi ya kuanza kwenye hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ni Agosti 13 fainali inatarajiwa kuchezwa na msako wa mshindi wa pili utafanyika palapale, Tanga.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Henock Inonga, Sadio Kanoute, Israel Mwenda, Mohamed Hussein.