KIUNGO MPYA AZAM FC ATOA KAULI YA KIBABE

KIUNGO mpya wa Azam FC Feisal Salum amesema kuwa anafurahia kuwa kwenye changamoto mpya ndani ya Azam FC.

Ni ingizo jipya ndani ya Azam FC akitokea kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi 2022/23.

Fei alipokuwa ndani ya Yanga alikuwa anavaa jezi namba sita anaendelea kuivaa pia akiwa ndani ya Azam FC.

Kiungo huyo anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoelekea kwenye kambi Tunisia kwa maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Nyota huyo amesema anafurahia maisha mapya na anatambua kazi itakuwa kubwa kwenye kutimiza majukumu mapya.

“Ninafurahi kuwa hapa na kupata changamoto mpya tunaamini tutafanya vizuri kufikia malengo yetu,” amesema.

Timu hiyo inatarajiwa kumenyana na Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 9 2023 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.