YANGA NDANI YA MALAWI SALAMA SALMIN

MSAFARA wa Yanga umewasili salama leo Julai 5 2023 kwa ajili ya mchezo maalumu wanaotarajia kucheza kesho Julai 6.

Timu hiyo imepewa mualiko maalumu na Serikali ya Malawi ambapo ni kwenye mchezo maalumu wa kutimiza miaka 59 ya Uhuru.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wapo kwenye kikosi hicho ni pamoja na Metacha Mnata, Clement Mzize, Dennis Nkane.

Mchezo wao wa kirafiki ni dhidi ya Nyassa Big Bullets kwenye mchezo huo maalum.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wanakwenda kuwakilisha taifa kimataifa.