WENGINE WATAMBULISHWA AZAM FC WAWILI

KHALIFA Ababakar Fall ametambulishwa kuwa kocha wa makipa na Ibrahim Diop ni mchambuzi wa mechi (Video Analyst), wote raia wa Senegal ndani ya Azam FC.

Ni Julai 3 makocha hao wametambulishwa ndani ya kikosi cha Azam FC kinachotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani.

Timu hiyo ipo kwenye maboresho ya kikosi hicho ambacho kimegotea nafasi ya tatu kwenye ligi baada ya kucheza mechi 30.

Ni Yanga waligotea nafasi ya kwanza na kutwaa ubingwa mbele ya Azam FC ambao walikuwa na mzunguko wa pili bora chini ya Kali Ongala ambaye alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi nane mfululizo bila kufungwa.

Yanga chini ya Nasreddine Nabi ilikusanya pointi 78 kwenye mechi 30 huku Azam FC ikikusanya pointi 59.

Makocha wote hao wamesaini kandarasi ya miaka mitatu.Tayari wachezaji wa Azam FC wameanza kuwasili kambini na kufanyiwa vipimo kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24.