CHUMA CHA AZAM KIMETUA BONGO

CHUMA cha pili kusajiliwa ndani ya Azam FC kimeweka wazi kuwa kimekuja Bongo kufanya kazi.

Tayari amewasili Bongo na kukamilisha taratibu za mwisho kwenye suala la kusaini dili jipya na timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za nyumbani.

Imegotea nafasi ya tatu kwenye msimamo na vinara wakiwa ni Yanga msimu wa 2022/23.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi ambapo walikomba pointi 78 na Azam FC ni pointi 59 walikusanya.

Ni Djibril Sillah ambaye anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa ndani ya Azam FC akiwa ni ingizo jipya mbali na wale ambao wamewaongezea mikataba.

Kiungo huyo alikuwa anakipiga Raja Casablanca hivyo msimu ujao atakuwa na uzi wa Azam FC.

“Nimekuja hapa kwa kuwa ninatambua nimekuja kufanya kazi na uwezo ninao kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu nina amini tutafanya vizuri,”.

Nyota wa kwanza kutambulishwa alikuwa ni Feisal Salum ambaye ni mzawa.