JEMBE LA KAZI BADO LIPO AZAM FC

MTAMBO wa mabao ndani ya Azam FC bado utaendelea kuwepo hapo baada ya kuongeza kandarasi ya mwaka mmoja.

Ni Idris Mbombo ambaye ana uwezo wa kufunga mabao akiwa nje ya 18 ama ndani ya 18 kwa wapinzani akiwa ndani ya uwanja.

Ni shuhuda timu ya Azam FC ikigotea nafasi ya tatu huku Yanga wakitwaa ubingwa wa ligi.

Yanga imetwaa ubingwa ikiwa na pointi 78 huku Azam FC nafasi ya tatu na point 59.

Taarifa kutoka Azam FC imeeleza namna hii:” Mshambuliaji wetu mahiri Idris Mbombo ataendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2024, baada ya kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja.

“Mbombo ni mmoja wa washambuliaji bora kwenye ligi yetu (NBCPL), kwenye misimu miwili iliyopita akiwa amefunga jumla ya mabao 17,”.