AZAM FC YAFUNGA MSIMU KWA USHINDI DHIDI YA POLISI TANZANIA

AZAM FC imeibuka na ushindi wa mabao 8-0 Polisi Tanzania ikiwa ni ushindi mkubwa kwa Azam FC msimu wa 2022/23.

Pia ni rekodi ya ushindi mkubwa ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 baada ya ubao kusoma Azam FC 8-0 Polisi Tanzania.

Ni Prince Dube katupia kambani dakika ya 8, 15, 28, 56, Kipre Junior amefunga dakika ya 20 Idd Suleiman katupia bao dakika ya 40 na 75 huku Yahya Zayd akitupia bao la kufungia ukurasa dakika ya 85.

Polisi Tanzania imeshuka daraja na msimu wa 2023/24 itashiriki Championship kupambania nafasi ya kurejea ndani ya ligi wakati ujao.