>

FEISAL NI AZAM FC MIAKA MITATU

FEISAL Salum, Zanzibar Finest anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa ndani ya Azam FC.

Nyota huyo anaibuka ndani ya Azam FC akitokea Yanga ambapo alikuwa na mkataba unaogotea ukingoni 2024.

Ni mkataba wa miaka mitatu amesaini ndani ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara pia Juni 12 itacheza fainali Kombe la Azam Sports Federation itakuwa dhidi ya Yanga.

Ikumbukwe kwamba nyota huyo alikuwa kwenye mgogoro na mabosi wake wa Yanga kutokana na suala lake la kimkataba ambapo alikuwa anahitaji kuondoka kwenye dirisha dogo.

Taarifa rasmi kutoka Azam FC imeeleza kuwa nyota huyo amepewa mkataba wa miaka mitatu huku wakitoa shukrani kwa Yanga kwenda nao sawa kwenye makubaliano.