>

YANGA WAPIGIWA GWARIDE LA HESHIMA

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City walipigwa gwaride la heshima.

Gwaride hilo Yanga walipigiwa kabla ya mchezo wao wa mzunguko wa pili dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Dakika 90 zilikamilikwa kwa sare ya kufungana mabao 3-3 na kugawana pointi tatu huku Yanga wakipindua meza kwenye mchezo huo.

Ni Mbeya City walianza kumtungua Eric Johora kipa namba nne wa Yanga ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi msimu wa 2022/23 lakini mwisho mabao yote yalirudishwa na kugawana pointi mojamoja.

Bado mchezo mmoja kwa Yanga kukamilisha mzunguko wa pili msimu wa 2022/23 ambapo watacheza dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 9 ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa timu hizo msimu wa 2022/23.