LEGEND kwenye masuala ya michezo kitaifa na kimataifa Saleh Jembe amewekwa wazi kuwa Yanga walikosa ubunifu kwenye mchezo dhidi ya USM Alger uliochezwa wa Mkapa Mei 28,2023.
Jembe amesema kuwa Yanga bado hawajamaliza mchezo na wana uwezo wa kupata ushindi kwenye mchezo wa pili ikiwa watafanya maandalizi mazuri huku akiweka wazi kuwa kama angeulizwa nani ambaye ni namba 10 amemtaja Feisal ambaye ana mgogoro na Yanga.