MASTAA wa Azam FC wameendelea na program maalumu kwa ajili ya kuwakabili wapizani wao Wagosi wa Kaya, Coastal Union kwenye mchezo wao ujao wa ligi.
Kwenye uwanja huo Azam FC wanatarajiwa pia kucheza mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation dhidi ya Yanga mchezo unaotarajiwa kuchezwa Juni 12.
Yanga ni mabingwa watetezi walitinga fainali kwa kuifungashia virago Singida Big Stars na Azam FC iliwaondoa Simba.
Azam FC chini ya kocha msaidizi Kali Ongala itamenyana na Coastal Union Juni 6 2023 ikiwa ni mzunguko wa pili kwenye ligi.
Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam 3-2 Coastal Union.
Kwenye mchezo huo bao la ushindi lilifungwa na Idd Suleiman, ‘Nado’ ambaye alianzia benchi na alipopata nafasi ya kuingia alifunga.
Mastaa hao ni pamoja na Nathan Chilambo, Bruce Kangwa, Keneth Muguna, Abdul Suleiman, ‘Sopu’, Pascal Msindo, Idris Mbombo, Malicou Ndoye, Tepsi Evance.
Mchezo uliopita Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Namungo FC , Uwanja wa Azam FC hivyo watawafuata Coastal Union wakiwa na hesabu za kuandika rekodi mpya.
Ongala amesema kuwa watafanya kazi kubwa kutafuta ushindi kwenye mchezo huo.
“Tunatambua umuhimu wa mchezo wetu ujao tutapambana kupata pointi tatu na inawezekana kwa kuwa kila mchezaji yupo tayari,”.