ROBERTO Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa miongoni mwa sababu zilizofanya wakagotea nafasi ya pili ni kuwa na wachezaji ambao hawapo fiti muda wote.
Miongoni mwa wachezaji ambao msimu wa 2022/23 ndani ya kikosi cha Simba walikuwa wanapambania hali zao ni pamoja na kiungo Peter Banda, Agustino Okra, Moses Phiri na Aishi Manula.
Simba imegotea nafasi ya pili kwenye msimamo na vinara ni Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Yanga imetwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 74 na imetinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Kuumia kwa Manula ambaye ni kipa namba moja wa Simba kulivuruga mwendelezo wa timu hiyo katika mataji matatu kuanzia ligi, Kombe la Azam Sports Federation na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Oliveira ameweka wazi kuwa kwenye mechi zote ambazo walikuwa wanacheza kikunwa ilikuwa ni kupata matokeo lakini wakati mwingine mambo yalikuwa tofauti.
“Ilikuwa ni kupata matokeo kwenye mechi zote ambazo tulikuwa tunacheza lakini bahati mbaya haikuwa hivyo, kuna wakati wachezaji walikuwa wanasumbuliwa na majeruhi hilo lilikuwa linatufanya tusiwe na mzunguko mkubwa wa kikosi.
“Nina amini kila mchezaji anapenda kuona tunapata matokeo hasa ukizingatia Simba ni timu kubwa na kila mchezaji anajituma kusaka matokeo kwa kilichotokea ni muda wa kujipanga kwa wakati ujao,” .