ROBERTO Oliveira raia wa Brazil ambaye anainoa Simba na Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambaye anainoa Yanga wamelipana kwa vitendo ndani ya dakika 90 kwenye mechi tofauti.
Ni Oliveira alianza kukiongoza kikosi chake Mei 12 ubao wa Uwanja wa Azam Complex uliposoma Simba 3-0 Ruvu Shooting nyota wake alibadilisha usomaji wa matokeo na kuwa ‘super sub’.
Ni Pape Sakho alitupia kambani mabao mawili akitokea benchi alichukua nafasi ya Jean Baleke dakika ya 60 alifunga mabao mawili dakika ya 72 na 90 kwenye mchezo huo.
Wakati Simba ikifikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 28 huku Ruvu Shooting ikishuka daraja mbinu za Rob zilijibu kwa mchezaji wake aliyeanzia benchi.
Ngoma ilijibiwa na Nabi, Uwanja wa Azam Complex Mei 13 ubao uliposoma Yanga 4-2 Dodoma Jiji, Mudhathir Yahya alifunga mabao mawili akitokea benchi alipochukua nafasi ya Aziz KI alifunga dakika ya 70 na bao la pili alifunga dakika ya 90 sawa na muda aliofunga Sakho.
Mbali na Mudhathir Clement Mzize naye alitokea benchi alipochukua nafasi ya Bernard Morrison alitoa pasi ya bao kwa Farid Mussa dakika ya 86 naye aliingia akitokea benchi alichukua nafasi ya Joyce Lomalisa.
Hivyo mbinu za makocha hao kwenye kubadilisha matokeo zilibadilika kutokana na wachezaji waliokuwa wakisoma mbinu na kupata ushindi.
Bingwa wa ligi ni Yanga huku Simba ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.