YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA SINGIDA BIG STARS

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa unahitaji pointi tatu kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Singida Big Stars unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti.

Mei 4, Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu ambazo Singida Big Stars nao wanazihitaji pointi hizo.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua uimara wa wapinzani wao hivyo watawakabili kwa tahadhari kupata pointi tatu.

“Kila mchezo kwetu ni muhimu kupata ushindi, tunatambua wapinzani wetu wanahitaji kushinda tunawaheshimu lakini nasi tunahitaji pointi tatu pia.

“Benchi la ufundi na wachezaji kiujumla wapo tayari kwa mchezo na tunaamini mbinu zitaleta matokeo mazuri kikubwa ni mashabiki kujitokeza na kushangilia timu yao bila kuchoka,” amesema Kamwe.

Yanga inapointi 68 ikiwa nafasi ya kwanza imecheza mechi 26 mchezo wa kwanza ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo huo Fiston Mayele aliandika rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi na alitoa pasi moja ya bao.

Mei 3 wachezaji wa Yanga walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo na miongoni mwao ni pamoja na Khalid Aucho,Mudhathir Yahya, Dickson Job na Kibwana Shomari.